Mpoto akirap mtakoma - Nay

01Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Mpoto akirap mtakoma - Nay

RAPA Nay wa Mitego amesema kuwa msanii wa kughani, Mrisho Mpoto, akiamua kufanya muziki wa hip hop hawezi kuwa na mpinzani, kwa madai kwamba ana uwezo mkubwa na ubunifu wa hali ya juu.

Mrisho Mpoto

Nay alisema kuwa Mpoto anafikiria na kuumiza kichwa anapoandaa kazi zake na anatumia akili nyingi, ndiyo maana yeye (Nay) akajiwa na fikra itakuwaje msanii huyo akiamua kuingia rap.

"Labda Fid Q ndiyo msanii pekee anayeweza kushindana naye, lakini ukweli ni kwamba jamaa huyu anafikiria, anaumiza kichwa anapoandaa kazi zake na anatumia akili nyingi sana ndiyo maana nikasema akifanya hip hop atakuwa hana mpinzani," alisema.

Nay alisema kuwa ameanza kujifunza kuiga mbinu za Mpoto na kuwashauri wasanii wenzake kufanya hivyo ili kuboresha kazi zao.