Linex akumbuka penzi la mzungu

28Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Linex akumbuka penzi la mzungu

KATIKA maisha ni watu wachache ambao huwa radhi kutoboa siri za mambo yao binafsi hasa wanapopitia katika changamoto mbalimbali hadi kufikia jamii kumuelewa vibaya.

Msanii wa Bongofleva, Sunday Mjeda ‘Linex’, ameamua kutoboa siri na kudai kuwa tangu ajitambue na kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na rafiki yake wa zamani ambaye alikuwa mzungu kutoka Finland, ndiye aliyemkuta katunza usichana wake.

Amedai kuwa hata kuachana kwao hakukuwa kwa ugomvi bali ni kutofautiana mahitaji na mrembo huyo.
“Unajua nchi za ukanda ule wa Scandnavia wanawake wanajitunza sana, na mzungu ndiye mwanamke pekee maishani mwangu niliyemkuta na bikra," amesema Linex.

Msanii huyo ambaye sasa ana wimbo wake mpya wa kwa hela, amesema bado anamkumbuka kimwana huyo wa kizungu kwa kile alichokikuta kwa mara ya kwanza walipoanza uhusiano wao.