Dully amesema mashaka yake ni kwamba uamuzi huo umechukuliwa na mapema na kufafanua kuwa itawawia vigumu wasanii wengi kuendana na utaratibu huo hasa ikizingatiwa kuwa walizoea mfumo wa zamani.
"Wasanii wangeendelea kuelimishwa kwanza ili kujua umuhimu wa kulipwa pale nyimbo zao zinapopigwa katika vyombo hivyo, lakini kwa hatua hii ya haraka haraka ninadhani kwamba sio nzuri," amesema Dully.
Dully amekiri kuwa hajawahi kuhudhuria semina wala vikao vyovyote vinavyohusu utoaji wa elimu juu ya sheria inayohusu haki ya msanii pale nyimbo zake zinaporushwa hewani, lakini amesema kuwa kwa maoni yake anafikiri hatua hiyo ingesubiri ili wasanii waelimishwe zaidi.










