Hiki nd'o kilichomvuta Baraka da Prince

10Feb 2016
DAR
Lete Raha
Hiki nd'o kilichomvuta Baraka da Prince

MSANII wa muziki wa kizazi kipya anayekuja kwa kasi, Baraka Andrew 'Baraka da Prince', amemtaja mtu aliyemvutia hadi akaamua kujiingiza kwenye muziki wa kizazi kipya kuwa Bob Rudala.

Baraka Da Prince

Baraka Da Prince amesema kuwa Rudala alimvutia kwa wimbo wake wa 'Nimekuchagua Uwe Wangu', aliotunga akiwa na bendi ya InAfrika, ambayo imekuwa ikipomorosha muziki nje ya nchi.

"Boby Rudaka alinivutia sana kwa wimbo wake huo nikawa ninatamani kuingia kwenye muziki wa kizazi kipya na hatimaye sasa na mimi nimekuwa na jina kubwa," amesema Baraka Da Prince.

Amesema kuwa kwa sasa mikakati yake ni mingi akiwa chini ya lebo aliyosaini mkataba hivi karibuni ya Tetemesha Records na kwamba hana budi kujali kile ambacho ameamua kukifanya.

"Nina mipango mingi ikiwamo ya kujitangaza zaidi nje ya mipaka ya nchi, tayari kuna kazi nimeshafanya na msanii wa Nigeria inaitwa Young King na kwa sasa tupo katika mazungumzo na Wizkid na kuna wimbo nimefanya na Jaguar aliyenishirikisha,” amesema.