Baada ya hapo ameendelea kupata umaarufu baada ya kuitendea haki video hiyo kwa kuchezwa na kuonyesha manjonjo.
Baadhi ya wasanii wengine walimuona 'Kidoa' akifanya vitu vyake kwenye video ya 'Akadumba' na kuamua kumshirikisha katika kazi zao ni Joseph Haule 'Profesa Jay' katika video yake ya 'Kamili Gado'.
Huyu si mwingine bali ni Video Queen Asha Salumu `Kidoa’, ambaye amesema kuwa anamheshimu 'Naye wa Mitego' kwa kumfungulia njia na sasa jina lake liko matawi ya juu.
Alisema umaarufu wake umeendelea kuongezeka kutokana na picha zake kali zinazoonyesha alivyoumbika kwenye mitandao ya kijamii.
"Nay wa Mitego amenifungulia njia na kuniweka matawi ya juu ingawa sasa nimekuwa ninakutana na changamoto mbalimbali zikiwamo za kusumbuliwa na wanaume kutokana na umbo langu," alisema Kidoa na kuendelea:
"Umbo langu linanipa wakati mgumu kiasi kwamba hata ninapokwenda kutafuta kazi lazima suala la mapenzi litazungumzwa," alisema.
Kimwana huyo alisema alichoamua kufanya sasa ni kwenda kwenye gym ili apunguze mwili..










