Ali Kiba aponda staili ya Diamond

10Feb 2016
DAR
Lete Raha
Ali Kiba aponda staili ya Diamond

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, ameendelea kurusha makombora gizani.

Ali Kiba

Mkali huyo wa Bongofleva, bila ya kumtaja mlengwa, amesema kuwa mtindo wa baadhi ya wasanii kutoa nyimbo mara kwa mara ni kutokujiamini na ni sawa na kuharibu kipaji.

Kauli hiyo imekuwa ikitafsiriwa na wengi kwamba inamlenga mpinzani wake, Diamond Platnumz, amekuwa akiachia ngoma kali baada ya nyingine, ambazo zimekuwa zikimpa tuzo mbalimbali.

Kiba amesema kuwa wasanii wanatakiwa kujipa muda wa kutoka badala ya kufululiza wakidhani kwamba mtindo huo utawasaidia na kumbe ni kujiharibia.

"Binafsi nikitoa kazi moja ina uwezo wa kukaa sokoni kwa muda mrefu kama ambavyo nyimbo zangu zilivyoshika chati ukiwamo wa 'Cheketua' ambao nina uhakika kwa mpenzi wa muziki wa kizazi kipya anaupenda," amesema Kiba ambaye ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la 'Lupela'.