Nuh amesema amefanya hivyo baada ya kugundua tabia halisi za Shilole ikiwa ni wiki chache tangu wamwagane na kudai kuwa Shilole ameingilia ukurasa wake wa Instagram, akimshambulia katika mahojiano mbalimbali, kitu ambacho kimemfanya kugundua kuwa msanii huyo alikuwa siyo rafiki yake.
Mbali na kuchora tattoo mpya juu ya ile ya Shishi Baby, msanii ameongeza tattoo nyingine kadhaa mwilini kwake, ikiwamo ya usoni, ikiwa ni ishara tosha kuwa naye sasa hana mpango na Shilole.










