Alisema kuwa wasanii wa hapa nchini wakiwamo wa muziki wa kizazi kipya na filamu wanaweza kufanya makubwa, lakini pamoja na uwezo huo bado kuna umuhimu wa kuwapo kwa nguvu ya serikali.
"Kuna mengi yanawezekana, lakini lazima kuwe na nguvu ya serikali kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za wasanii wa Tanzania ili waweze kufikia malengo waliojiwekea katika sanaa," alisema Kiba na kuongeza:
"Mfano mzuri ni kile ambacho wasanii wa Watanzania Single Mtambalike ‘Rich Rich’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’ walichokifanya katika tuzo za African Magic People’s Choice Awards zilizofanyika hivi karibuni huko Nigeria."
Alisema kuwa nchi ina vijana wengi wenye vipaji ambao hawajatoka, hivyo zinahitajika juhudi za makusudi za kuwasaidia ili nao waweze kupiga hatua ili kufikia mafanikio.










