Alisema kuwa alikuwa miongoni mwa wasanii walioshiriki katika kampeni hizo kwa upande wa CCM na kulazimika kuahirisha masomo na sasa anajipanga kuendelea.
"Ilikuwa nimaliziea masomo ya sekondari mwaka jana, lakini kutokana na shughuli za kampeni nililazimika kukatisha masomo na sasa ninajipanga ili niendelee na shule," alisema Kazinja.
Msanii huyo ambaye alitamba kwa mara ya kwanza kupitia wimbo wa 'Presha' aliomshirikisha Banana Zorro, alisema ameandaa wimbo mpya ambao hautaji kuhofia kuibiwa 'idea'.










