Msanii huyo aliiambia East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo kuwa ameingia Radar Entertainment na kuachana na Wanaume Halisi, lakini anaonekana kumkwaza Nature.
“Nilikuwapo ndani ya kundi la Wanaume Halisi, sasa labda anavyoona mi nipo huku ina maana anaona kazi zake tena zitakuwa zinalega lega, pengine labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mimi nifanye kazi naye, siku zote wanasema watu ni kubadilisha mazingira, kubadilisha sanaa, kikubwa aniache nitingishe tu," alisema KR Mullah.
Msanii huyo alifunguka hayo baada ya Nature kusema kitendo cha KR kujiunga na Radar Entertainment, huenda kitamharibu asipokuwa makini.










