Akizungumza na gazeti hili, Muumin alisema uzinduzi huo umeahirishwa kutokana na sababu zilizo juu ya uwezo wa uongozi wa bendi hiyo na hivyo wanamuziki wanaendelea kujipanga zaidi.
"Tulipanga kuzindua rasmi bendi yake mwezi Septemba na kisha Desemba tungezindua albamu mbili kwa mpigo, lakini zimejitokeza sababu ambazo ziko juu ya uwezo wetu, hivyo tumeahirisha," alisema Muumin.
Alisema, tangu Januari mwaka huu, bendi hiyo ilikuwa ikiandaa wimbo mmoja kila mwezi na kufankiwa kukamilisha nyimbo sita zikiwamo za 'Yatima Mzee, Mwanangu, Fenesi' na 'Kwa Mparange Sihami'.
"Mwanzoni mwa Juni mwaka huu tulitambulisha wimbo wa Mkonga wa Tembo kwenye onyesho letu tulilolipa jina la White Part na sasa kilichobaki ni kusonga mbele ni harakati za kurejesha heshima ya dansi nchini," alisema.
Aidha, Muumin alisema, katika moja ya mikakati yake ni kushirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wa ndani na nje ya nchi, kwenye baadhi ya nyimbo za bendi hiyo ili kupata vionjo tofauti.
"Ninatamani kumshirikisha msanii wa muziki wa kizazi kipya kama Jose Chamilione wa Uganda katika nyimbo zetu za baadaye na wengine wa Tanzania kama Zuchu, Nandy na wengine," alisema.
Alisema, muziki kwa sasa umebadiliko, hivyo wao kama Special Band, hawana budi kwenda na mabadaliko hayo ili kujizolea mashabiki wengi zaidi wa rika mbalimbali wakiwamo watu wazima na vijana.










