Kamishna wa Mkoa Kitengo cha Uhamiaji, John Msumule Mwanambilimbi, ambaye bendi yake ina mkataba wa kutumbuiza Hoteli ya Giraffe anadaiwa kuwatumia raia wawili Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Kashama Alan Mulumba na Mwanabantu Kibyabya Michel.
Alisema Mulumba alikuwa na hati ya kusafiria ya zamani yenye namba C0172419 iliyotolewa Juni 12 mwaka 2008 na kuisha Juni 11, mwaka 2011 na nyingine mpya yenye namba OBO782268 iliyotolewa Aprili 21, mwaka jana inayoonyesha kuisha mwaka 2014/2020.
Alisema Kibyabya alikutwa na hati ya kusafiria namba OBO487018 iliyotolewa Machi 29, mwaka 2008. Alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani wiki ijayo.










