Kama ilivyo kawaida yake muimbaji huyo wa dansi ya kuwashirikisha wasanii mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya, safari hii ameshirikiana na Joh Makini na G Nako wa Kundi la Weusi kutoka jijini Arusha.
"Kama kawaida yangu wimbo huo upo kwenye mtindo wa rhumba ingawa ndani yake kuna wasanii hao wa Hip Hop, lakini cha muhimu ni kwamba imekamilika na uko vizuri sana," alisema Bella na kuendelea:
"Bado ninaendelea na kazi ya kushuti video yake ambayo kama nilivyosema inaweza kukamilika mapema sana mwezi huu na nitaiachia ianze kusikika ili mashabiki wangu waisikie kwani niko katika hatua za mwisho."
Muimbaji huyo alifafanua kuwa hawezi kusema kibao hicho ni bora zaidi ya vingine, kwa madai kwamba kila shabiki ana upokeaji wake kulingana na kibao kinavyomgusa kwa kusikiliza mashairi yake.









