Msanii huyo alisema sababu ya kushindwa kutoa kazi za kutosha kwa mwaka 2015 ni kusuasua kwa soko la filamu nchini.
"Mwaka huu wa 2016 utakuwa mzuri kwangu kwa sababu tayari nina kazi nyingi ambazo sijazitoa, hivyo nitakuwa ninaangusha moja baada ya nyingine," alisema Kajala.
Alisema kuwa kilichobaki kwake ni kujipanga tu licha ya kuwapo kwa changamoto za wezi wa kazi za wasanii.










