Beyonce, Kelly kuwajengea nyumba maskini

10Jul 2023
Nipashe
Beyonce, Kelly kuwajengea nyumba maskini

WANAMUZIKI wawili waliokuwa wakiunda kundi la Destiny’s Child, wameishangaza dunia baada ya kutangaza kujenga nyumba 31 kwa ajili ya kuwasaidia watu wasiokuwa na makazi.

Wasanii hao, Beyonce na Kelly Rowland, watajenga nyumba hizo katika kaunti ya Harris katika eneo la Midtown la Houston.

Aidha, sehemu ya pesa hizo kiasi cha dola milioni saba zitapelekwa katika makazi ya Knowles-Rowland kama mpango wa uokoaji wa Marekani.

“Kaunti ya Harris na jiji la Houston, kwa pamoja na muungano wa watu wasio na makazi, wamepunguza ukosefu wa makazi katikati ya janga hilo kwa asilimia 20, na tumeweza kushikilia upungufu huo,” Jaji Lina Hidalgo amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Ameongeza “Ni mipango kama hii ambayo hakika nitaiunga mkono bila kujali ni nani aliye nyuma yake, lakini inavutia sana, nadhani, kwa sababu kuna majina haya ya Beyoncé na Kelly Rowland, bila shaka, wamekuwa wakiunga mkono. jamii kwa muda mrefu sana.”

Hidalgo mesema kuwa uzinduzi utatangazwa wakati wa tamasha la Renaissance World Tour itakapofanyika Oktoba huko Houston.