Chameleone bado hali tete

09Jul 2023
Na Mwandishi Wetu
Nipashe Jumapili
Chameleone bado hali tete

HALI ya mwanamuziki mahiri kutoka Uganda Jose Chameleone, inaelezewa kuwa mbaya baada ya kukabiliwa na tatizo la tumbo ambalo linamsababishia maumivu makali.

Jose Chameleone.

Baba mzazi wa mwimbaji huyo, Gerald Mayanja amethibitisha kuwa mtoto wake anaugua ugonjwa huo tangu ahamishie makazi yake nchini Marekani.

“Chameleone amekuwa mgonjwa katika miezi iliyopita. Alipohamia Amerika, ugonjwa ulizidi kuwa mbaya. Sasa ni mgonjwa sana, yuko kwenye kitanda chake cha wagonjwa. Amekuwa akipata matatizo ya tumbo ila kwa sasa anapokea matibabu,” Mzee Mayanja ameiambia Bukedde Tv.