Alikiba kapata ahueni YouTube

25Jun 2023
Dar es Salaam
Nipashe Jumapili
Alikiba kapata ahueni YouTube

YAWEZEKANA staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba, amepata ahueni baada ya akaunti yake ya Youtube, kurudishwa na watekanyara wa mitandao, lakini kuna wasiwasi kawekewa mtego.

Ali Kiba.

Awali akaunti hiyo ilidukuliwa na kushikiliwa na mtu aliyejiita TESLA INC, huku video zote zikiwa zimefichwa na hakuna mtu aliyefanikiwa kuzifikia.

Mbali ya video hizo kurudishwa bado kuna video moja ambayo sio ya Alikiba inaonyesha ikitumiwa na ile akaunti ya mwanzo ambayo walienda mubashara kupitia akaunti hiyo.