Rapa Big Pokey afariki dunia

19Jun 2023
Nipashe
Rapa Big Pokey afariki dunia

RAPA wa Marekani Big Pokey, amefariki dunia baada ya kuzimia wakati wa onyesho huko Texas.

Milton Powell.

Msanii huyo, ambaye jina lake halisi ni Milton Powell, alikuwa akitumbuiza katika hafla yenye mada ya ‘Juneteenth’ kwenye baa moja siku ya Jumamosi alipoanguka chali jukwaani.

Mashahidi walikimbia kumsaidia kijana huyo mwenye umri wa miaka 45 kabla ya kupelekwa katika hospitali iliyo karibu. Na alifariki dunia jana Juni 19, 2023.