Ally Choki: Kumiliki bendi ni hasara

12Jun 2023
Sabato Kasika
Dar es Salaam
Nipashe
Ally Choki: Kumiliki bendi ni hasara

​​​​​​​MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi, Ally Choki amesema kumiliki bendi kumesababisha maisha yake kuyumba.

​​​​​​​MWIMBAJI nyota wa muziki wa dansi, Ally Choki.

Amesema kumiliki bendi ni gharama kubwa, na kwamba alijaribu mara mbili na kujikuta akipata hasara ambayo huenda angekuwa na maisha mazuri akimiliki mali nyingine nyingi.

"Wamekuja watu wengi tu kunishawishi kuwa nianzishe bendi, ukweli ni kwamba bendi imekwamisha maendeleo yangu," alisema Choki.

Alifafanua kuwa wanamuziki ni kama watoto wadogo, kwa maelezo kwamba wanapenda kudekezwa.

"Wanataka wafanyiwe kila kitu, halafu kila mara ni malalamiko tu ya kutaka kusaidiwa fedha, katika mazingira hayo, bendi haiwezi kupiga  hatua na hata mmiliki wake hawezi kufanya maendeleo yake," alisema.

Aidha, alisema muziki wa dansi unazidi kushuka kwa madai kwamba mameneja wa vipindi vya muziki katika vyombo vingi vya habari ni vijana.

"Kimsingi, umri wao ni wa vijana wetu, kwa hiyo wanapenda muziki wa vijana wenzao kuliko dansi," alisema.