Rais alivyotumia Ripoti CAG kuthibitisha kukubalika,uwazi,uwajibikaji

12Apr 2023
Na Mwandishi Wetu
DAR ES SALAAM
Nipashe
Rais alivyotumia Ripoti CAG kuthibitisha kukubalika,uwazi,uwajibikaji
  • Kilichoamuliwa TRC yawa darasa aina yake

NI ngumu sana kwa wataalamu wa siasa wanaeleza katika namna ya kutenganisha siasa na mwenendo wa uchumi na mara zote huwa zinategemeana. Siasa mara zote huamua jambo, huku uchumi ukiwa unaendesha hali halisi na maisha ya kila siku.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea Taarifa ya Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2021/2022 kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Charles Kichere, Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 29 Machi, 2023.

Wanasiasa hushikilia nyendo hizo, nguvu kuu ikiegemea penye undani wa uchumi. Nchini hadi sasa, kuanzia maisha ya kijamii na hata kisiasa, mada inayotawala kwa kiasi kikubwa ni Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali (CAG) ya mwaka 2021/22  , iliyotolewa siku chache zilizopita. Ni suala la fedha na uchumi, ikikamata nguzo ya kisiasa nchini.

Mara tu baada ya ripoti hiyo ambayo akamwasilishia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye naye anatolea ufafanuzi wa majibu na uamuzi, pasipo ‘kuyakopa’ bali akayafafanua kwa kina undani wake na mwelekeo wa kiserikali.

Dk. Samia akaeleza papo kwa hapo penye kasoro, akinena kwa tafsiri yenye kubainisha maeneo ambayo walakini ukitajwa. Pia, ni aina ya maelezo ambayo yanabeba sura ya kina katika mustakabali mkuu, umma ukishuhudia msimamo wa kirais kwa umma; uwajibikaji, uwazi, pia lugha na matendo ya kukubalika kwa umma.

Suala la uwazi unaanzia pale, CAG safari hii na hata mwaka uliopita awasilisha hilo katika mustakabali huo faragha kwa umma, kupitia vyombo hai vya habari ni maslahi ya umma na wanapaswa kujua.

Lakini katika hatua hiyo ya kwanza, nayo ikabeba sura nyingine ya pili ni pale Rais Dk. Samia akionyesha namna ya kuwajikibika, kuanzia taarifa ya awali pale Rais alipoonyesha baadhi ya maeneo kutokukubaliana na ‘uchafu’; ulioanikwa na CAG na Rais Dk. Samia akiungana naye kukiri kuna uchafu.’

Ni mara moja, ripoti mpya ya CAG inaibua uwakibikaji unaochukua nafasi, ikirejewa katika uamuzi wa rais wikiendi iliyopita kuvunja Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa juu, akiungana na hoja ya CAO katika shirika hilo.

Kwa mujibu wa CAG, kuzidishwa muda wa mikakati ya mradi wa reli ya kisasa (SGE) unaendelea sasa, umekuwa na atahari ya kwanzs ni gharama kubwa, ukiwa umezidi kwa miaka kadhaa.

Vyama vya siasa kama kawaida yao havikukaa kimya, navyo vikaanza mara moja kuitoa  michango yao kuhusu hoja na tukio hilo. Vilevile wadau nje ya vyama, wanaojumuisha wasomi na taasisi binafsi, vyote kwa pamoja vimekubaliana na hatua ya Rais Dk. Samia kwamba amekubalika.

Msingi wake huo pekee ni kwamba, ukaonekana kuwa hatua mbele ya Rais lakini ikavuka na kikubwa ambacho kinatokana na mchango wa umma wote tajwa, unaendelea hadi sasa, mfano ni baadhi ya wadau wakitaka kuwapo hatua zaidi, kulingana na hatua tajwa na CAG. Tayari vyama kama ACT Wazalendo na Chadema, vimeshanena yao, hali kadhalika taasisi binafsi.

Ujumla wake, unaibua mwelekeo bora katika taarifa hizo za CAG, ambazo zinaunda hata utamaduni na mwenendo sahihi katika dhana nzima ya sayansi ya uchumi, katika mustakabali mpana kama uwajibikaji, uwazi na kukubalika.