Akizungumza mara baada ya pambano hilo kumalizika, Mingange alisema kuwa refa huyo tangu mechi ilipoanza alikuwa akiwatoa mchezoni wachezaji wake kwa maamuzi ya ajabu na hata goli la kwanza lilipatikana baada ya mchezaji wake John Mahundi kufanyiwa rafu ambayo hakupiga filimbi.
"Sisi makocha sasa tunaonekana hatuna maana, sasa kuna sababu gani ya kufundisha, mtu unafundisha halafu anakuja mtu mmoja na kuamua nani ashinde mechi, hii si haki kabisa," alisema kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC.
Kocha huyo pia alisema matukio mengine ambayo yanaonyesha kuwa mwamuzi huyo alikuwa ni kama alikuwa anachezesha kwa maagizo, ni kitendo cha kumpa kadi nyekundu beki wake Tumba Swedi na kuwaacha Haruna Moshi 'Boban' na Kelvin Yondani waliopigana uwanjani bila kuwapa adhabu yoyote ile.
"Sijui alitumia kigezo gani kumpa Swedi kadi, lakini kawaacha Boban na Yondani wamepigana mbele yake, lakini hakuchukua hatua yoyote na inawezekana kwa sababu tu ingewaathiri Yanga kama beki huyo angetoka ndiyo maana hakutoa kadi," alisema Mingande kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa anachojua kama ni busara ingetumika kwa Swedi kwa sababu aliruka na mchezaji wa Yanga kugombania mpira, lakini Yondani na Boban walizipiga kavu kavu kila mtu akiona.
"Sasa wale waliogeuza soka ni masumbwi wanaachiwa, yule aliyefanya kosa la kimpira anatolewa nje kwa kadi nyekundu, huu ni uamuzi wa aina gani?" Alilalamika kocha huyo.
Hata hivyo, alidai kuwa huenda ulikuwa ni mpango uliopangwa kutokana na kuhofia historia yake wakati akiwa Ndanda FC kwani hakuwahi kufungwa na Yanga msimu uliopita alipoilazimisha sare ya bila kufungana uwanja wa Taifa na kushinda bao 1-0 nyumbani mjini Mtwara.
"Nadhani hili liliwatisha, lakini mimi nawaambia Yanga ni timu nzuri inaweza kushinda bila kubebwa, waamuzi waache tabia hii," alisema.
Waamuzi waliibeba Yanga - Mbeya City
31Dec 2015
Taifa Letu
Waamuzi waliibeba Yanga - Mbeya City
KOCHA mkuu wa Mbeya City Abdul Mingange amesema kuwa mwamuzi Jonisia Rukya aliwabeba wapinzani wao Yanga kwa mbeleko ya chuma, kiasi cha kusababisha kupoteza mechi hiyo kwa mabao 3-0 Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa Yanga na Mbeya City wakiwa uwanjani jijini Dar es Salaam.









