Akizungumza jijini Dar es Salaam Aveva alisema kuwa litakuwa ni jambo jema kwa sababu soka la sasa linahitaji zaidi fedha, tofauti na zamani ambalo lilikuwa ni kama la kujitolea tu.
Hata hivyo, alisema jambo hilo linahitaji muda, tathmini na umakini wa hali ya juu kwa sababu ni klabu ya wanachama ambayo katiba yao bado haisemi au haina kipengele chochote kinachowataka wafanye hivyo hadi pale itakapobadilishwa.
Kingine ni kuutoa umiliki kutoka kwa wanachama na kuupelekea kwa wanahisa jambo ambalo linatakiwa kufanyika kwa umakini na uweledi wa hali ya juu.
"Unajua kwa sasa soka limebadilika kutoka kwenye ridhaa na kuwa la kulipwa, zamani wachezaji walikuwa wanafanya kazi kwenye kampuni na mashirika mbalimbali kwa hiyo kulikuwa hakuna kambi, siku hizi wachezaji mpira ni ajira, wanakaa kambini kwa hiyo klabu zinatumia gharama kubwa, sasa ni lazima twende na wakati vinginevyo hatuwezi kufika," alisema Rais huyo na kuongeza.
"Lakini pamoja na hayo, Simba ni klabu kubwa yenye wanachama wengi na moja ya thamani yao ni umoja wao na nguvu, hivyo ni lazima kwanza kila kitu kifanyike kwa umakini wa hali ya juu, kuanzia kwenye tathmini ya thamani ya klabu yenyewe, pamoja na kubadilisha katiba ili iendane na matakwa ya kisasa na mengine mengi ambayo yanahitaji weledi na umakini wa hali ya juu, kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwamo wathamini, wanasheria na wanachama na wadhamini wa klabu," alisema.
Kutokana na maelezo hayo inaonekana pamoja na uongozi wa Simba kukubaliana na klabu kujiendesha kisasa, lakini jambo hili linaonekana huenda likachukua muda mrefu kutokana na mlolongo jinsi ulivyo.
Mo ambaye ni mwanachama wa klabu hiyo alisema kuwa angependa kununua hisa zinazozidi asilimia 50 ili aweze kupata haki ya kuiendesha klabu hiyo na kuifanya kijiendesha kisasa na kuweza kushindana na klabu kubwa Afrika kama TP Mazembe, Zamaleki, Al Ahly, Etoile du Sahel na nyingine nyingi.
Aveva akubali Mo kununua Simba
31Dec 2015
Taifa Letu
Aveva akubali Mo kununua Simba
RAIS wa klabu ya Simba Evance Aveva amekubali ombi la mfanyabiashara Mohamed Dewji kutaka kununua hisa zaidi ya asilimia 50 ndani ya klabu hiyo.
RAIS wa klabu ya Simba Evance Aveva









