Niyonzima ambaye pia ana mashabiki wake binafsi kutokana na aina yake ya uchezaji inayowakuna wengi, pia ameitakia mafanikio mema timu yake kwenye mechi za Ligi Kuu inayoendelea
“Yanga ni timu yangu na nimeishi nayo vizuri pamoja na watu wake, lakini sina furaha kuwa nimekaa nje kwa muda usiojulikana au kuwa pembeni ya timu lakini haya yote ni majaribu na najua ni vitu ambavyo vipo duniani ila naamini yataisha vizuri tu”, alisema Niyonzima na kuongeza.
“Mimi ni binadamu naweza kufanya makosa lakini nawahakikishia wapenzi wa Yanga na Niyonzima kwamba hili litaisha siku si nyingi na wataendelea kupata burudani kama ilivyokuwa au hata zaidi, aliendelea kusema na kusisitiza.
"Pia nawatakia wana Yanga 'Merry Christmas na Happy New Year', tumalize mwaka kwa amani, tuanze mwaka 2016 kwa amani, kwa wapenzi wa Haruna pia kwa watanzania wote”.
Kiungo huyo raia wa Rwanda amesimamishwa kwa muda usiojulikana na uongozi wa Yanga kutokana na kuchelewa kurudi kujiunga na timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Challenge Cup 2015 michuano iliyomalizika hivi karibuni nchini Ethiopia.
Niyonzima atoa zawadi Yanga
31Dec 2015
Sema Usikike
Niyonzima atoa zawadi Yanga
KIUNGO maridadi wa Yanga Haruna Niyonzima ametoa zawadi ya salamu za heri ya Krisimasi na mwaka mpya kwa wanachama na mashabiki wa klabu yake na kuwataka kuwa wavumilivu kwani suala lake linatarajiwa kupatiwa ufumbuzi hivi karibuni baada ya kuwasilisha maelezo kwa uongozi.
Haruna Niyonzima










