Ahly – mabingwa wa mara nane wanaofundishwa na kocha wa zamani wa Tottenham ya England, Martin Jol walishindwa kutamba mbele ya wenyeji wao waliotawala sehemu kubwa ya mchezo.
Zesco United, ambao hawajawahi kuvuka zaidi ya hatua ya makundi ya michuano ya Afrika, walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kiungo John Chingandu katika dakika ya 27, kabla ya Ahly kusawazisha dakika tatu baadaye kupitia mshambuliaji wakimataifa raia wa Ghana, John Antwi.
Dakika tano ndani ya kipindi cha pili, wenyeji walirejea na makali na kufunga bao la pili likiwekwa kwenye kamba na Clatous Chama na dakika sita baadaye Zesco walifanya matokeo kuwa 3-1.
Ahly walipambana kiume na kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 67 likipachikwa kwenye kamba tena na mshambuliaji Antwi.
Kadhalika, katika mechi ya Kundi A, Wydad Casablanca, waliowaondoka kwenye michuano mabingwa watetezi, TP Mazembe walianza kampeni na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast waliokuwa kwenye uwanja wa nyumbani.
Timu hiyo ya Morocco waliokuwa washindi wa pili msimu uliopita, walipata bao la ushindi katika dakika ya 39 kupitia kwa
mshambuliaji, Salah Eddine Saidi.
Aidha, mabingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika, Etoile du Sahel nao wameanza kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Kawkab Marrakech ya Morocco Ijumaa iliyopita.










