Wachezaji hao ni kama Donald Ngoma na Wazimbabwe wenzake Thabani Kamusoko anayeichezea pia Yanga, Justice Majabvi ambaye yupo Simba, Vicent Angban na Juuko Murshid wa Simba, Kipre Tchetche, Amissi Tambwe wa Yanga na wengineo.
Hata hivyo, kuna wachezaji wa kigeni ambao hawakufanya vizuri kwenye Ligi Kuu msimu huu.
Kuna wachezaji ambao walikuja nchini kama vile kuchuma fedha tu, lakini hakuna chochote walichokifanya si kuzisadia klabu zao au hata kufurahisha mashabiki.
1. Pape Abdoulaye Ndaw-Simba
Kama kitaundwa chama cha wachezaji waliochemsha msimu uliomalizika 2015/16, huyu ndiye alifaa kuwa mwenyekiti wao.
Aliongoza kwa kuchemsha zaidi msimu huu. Stori yake inachekesha, inahuzunisha, inashangaza, inaudhi na kukera kwa wakati mmoja.
Haikuwa hivyo. Akaanza kuwa kituko. Kuanzia urefu wake kama mcheza mpira wa kikapu, uchezaji wake uwanjani mpaka vituko vyake.
Moja ya vituko vyake vya kukumbukwa ni viatu vyake vichakavu alivyochezea kwenye mechi moja ya Ligi Kuu.
Pia kwenye mechi moja dhidi ya Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine alikutwa na kitu kinachofanana na hirizi.
Hadi mkataba wake unasitishwa kwenye kipindi cha dirisha dogo msimu huu, hakuwahi kufunga goli hata la kuotea.
2. Issoufou Boubacar-Yanga
Huyu huwezi kumlinganisha sana na Ndaw. Nadhani kilichomgharimu raia huyu wa Ghana kuichezea timu kubwa kama Yanga iliyosheheni wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.
Pamoja na kusababisha goli kutokana na krosi yake maridadi iliyomfanya beki wa Al Ahly ajifunge kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini bado hakujihakikisha namba kwenye kikosi hicho hata kwenye Ligi Kuu tu.
3. Allan Wanga-Azam
Haijulikani naye amepatwa na kitu gani. Msimu mmoja uliopita kabla ya kujinga na Azam FC aliwafunga magoli mawili kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa kwenye mechi ya ugenini dhidi ya El Merreikh ya Sudan.
Nadhani hiyo ndiyo ilikuwa sababu ya vibopa na benchi la ufundi kumsajili.
Lakini tangu alipojiunga na klabu hiyo msimu wa 2015/16 hakuna lolote la maana alilofanya na mpaka ligi msimu huu unamalizika alikuwa amefunga magoli mawili tu.
4. Brian Majegwa-Simba
Simba ilijibebea mchezaji huyu kutoka Azam. Labda kutokana na urahisi wa bei.
Tangu alipojiunga na Simba kwenye kipindi cha dirisha dogo msimu uliomalizika, hajaonekana kufanya lolote la maana zaidi kufunga goli moja tu.
5. Paul Kiongera-Simba
Alisajiliwa na Simba akitokea KCB ya Kenya msimu wa 2013/14.
Akaonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi za kirafiki na kwenye mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal kabla ya kuumia.
Akiwa huko Mkenya huyo, alionyesha kiwango kizuri na kuwafanya wanachama na mashabiki wa Simba waulazimishe uongozi kumrejesha kwenye kipindi cha dirisha dogo.
Tofauti na matarajio yake, alichokuwa akikifanya anakijua mwenyewe.
6. Michael Ballou - Azam
Si mchezaji mbaya sana, lakini si aina ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa nchini.
Uwezo wake ni wa kawaida ambao wachezaji wengi viungo wa Kibongo anaweza kucheza tofauti na pacha wake Kipre Tchetche.










