Linah: Sikimbilii kuwa mama

01Jun 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Linah: Sikimbilii kuwa mama

NYOTA wa muziki wa kizazi kipya, Linah Sanga, amesema kuwa hana haraka ya kuzaa kwa vile suala la kuwa mama linahitaji kujipanga siyo kukurupuka tu kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakifanya.

Linah Sanga

Msanii huyo alisema kuwa kutopata mtoto mapema haina maana kwamba ana matatizo yoyote ya uzazi bali ni malengo tu ambayo amejiwekea katika maisha yake.

Linah amekiambia kituo kimoja cha redio kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakimsakama na kuuliza kwa nini hana mtoto huku wengine wakidai kwamba ana matatizo ya uzazi.

Alisema suala la kuolewa, kuzaa na kuwa na familia ni jambo muhimu kwa kila binti, lakini yote yanapaswa kuja kwa wakati mwafaka.