Mgogoro wa uchinjaji Kimara na bei ya nyama inavyopaa

27May 2016
Efracia Massawe
Dar es Salaam
Nipashe
Mgogoro wa uchinjaji Kimara na bei ya nyama inavyopaa

Ni miaka mitatu imepita sasa, tangu kuwapo mgogoro kaatika Machinjioni ya Mifugo ya Kimara, jijini Dar es Salaam
Hali inayofanana na hiyo, ndiyo ilikuwapo katika machinjio ya Vingunguti, hadi ukafungwa. Umefunguliwa wiki kadhaa zilizopita.

Ng’ombe waliofikishwa katika Machinjio ya Kimara Suka na kisha wanahamishiwa katika machinjio mapya, kama Tegeta na Kimara Stop Over. (PICHA: EFRACIA MASSAWE)

Mgogoro wa machinjio ya Kimara, katika awamu ya kwanza, ulihusu uhalali wa kuchinja ng’ombe kati ya waumini wa imani mbili tofauti, lakini baadaye ulipatiwa ufumbuzi kwa maafikiano baina ya wahusika hao.

Wakati hilo limeisha, machinjio hayo yanakabiliwa na fukuto la mgogoro unaofika mbali hadi kwa mnunuzi kuuziwa nyama yenye bei kubwa.

Hilo ni tatizo ambalo katika sura pana, linahusu machinjio mengi ya ndani na nje ya Dar es Salaam. Kwa ujumla, hayakidhi vigezo vya mazingira, afya na biashara. Si salama kwa wakazi jirani ma hata wachinjaji wenyewe.
Pia katika taratibu za ndani kuna mianya inayozaa migogoro mingi machinjioni.

MGOGORO WA WACHINJAJI
Miongoni mwa wafanyabaishara waliongia katika malumbano na serikali, ni Umoja wa Wafanyabiashara wa Mifugo na Mazao wa Kinondoni Dar es Salaam.

Wakiwa wamepanga wamejipanga kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, kueleza changamoto zinazowakabili, dai lao ni manispaa hiyo kuwazuia kuendelea na shughuli za uchinjaji katika Machinjio ya Kimara Suka, kwa dai la wanakiuka Sheria ya Uchinjaji.

Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, amadhan Dule, anasema mgogoro na manispaa ni wa muda mrefu kutokana na wao kupinga kulipa Sh. 18,500, badala ya 12,000, walizokuwa wakitoa kwa kila ng’ombe.

Anasema ng’ombe hao baada ya kutoka mikoani huwafikisha Ruvu nje kidogo ya Dar es Salaam, kwa lengo la kupewa alama ya muhuri kwa Sh. 6,500 kama mifugo inayochinjwa.

Anasema mbali na kutozwa Sh. 5,500 kwa kila ng’ombe ili kupata kibali na daktari wa kupima nyama hiyo, lakini manispaa inawalazimisha, mifugo hiyo ikakae machinjio ya Pugu na kila mmoja hutozwa Sh. 6,500 na gharama nyingine za kuisindikiza mifugo kutoka Kimara.

Dule anadai ni mgogoro uliosababishwa na utendaji usio sahihi kwa maofisa wa manispaa, kwa kutaka wafanyabiashara watozwe gharama waanazodai ‘ni za ziada.’

“Kwa mantiki hiyo tumejipanga kukutana na Mkurugenzi wa Manispaa (Kinondoni), kutafuta umfumbuzi,” anasema Dule.

Machinjio hayo yaliyofungwa kwa miezi miwili sasa, yanadaiwa kuipotezea manispaa mamilioni ya shilingi kutokana na ushuru mbalimbali.

Diwani wa Kata ya Saranga, iliko machinjio hayo, Ephrahim Kinyafu, anasema mgogoro ulipaswa kutatuliwa mapema. Anafafanua:

“Labda jambo la kuangalia kwa sasa ni manispaa kuungana na watu wa wizara kutzama kwa pamoja, namna athari inavyoendelea kujitokeza na ikiwezekana suala hilo lifikie muafaka mzuri.”

Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli, anakiri kupata taarifa ya mgogoro wa Kimara na yuko katika hatua ya kukutana na Umoja Wachinjaji, ili kuangalia namna ya kuutatua.

Mgogoro mwingine kama huo, ni uliotatuliwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi, ukihusu Chama cha Wafanyabiashara Mifugo na Mazao Yake Vingunguti (Uwamivi Society).

Hata hivyo inasadikika kuwa migogoro mingi imechangiwa na viongozi wa serikali kutokuwa makini katika kupokea taarifa za kero za makundi husika na namna ya kuzifanyia kazi.

Matokeo ya migogoro hiyo imefanya bei ya nyama kupanda zaidi kutokana kuwapo ushuru wa aina nyingi.
Umoja wa Wafanyabiashara wa Mifugo na Mazao wa Kinondoni, wamesema hawako tayari kutoa ushuru mara mbili, kama ilivvyokuwa hadi machinjio yakafungwa.

Wanala,amika kuwa, Sheria ya Kuzuia Magonjwa ya Mlipuko na Uangalizi wa Ng’ombe, inatumiwa vibaya na maofisa wa Manispaa ya Kinondoni.

“Awali tulikuwa tukisafirisha ng’ombe zetu kwa njia ya treni. Tulikuwa tukizipeleka kambi ya jeshi na Tanganyika Packers. Tunaungana wafanyabiashara wengine ikiwamo, Kambi la Jeshi, tunakodi behewa la treni kwa ajili ya kusafirisha ng’ombe hadi Dar es Salaam,”anasema mfanyabiashara mmoja.

Mmoja wa wachinjaji 35 waliokuwa wakifanya kazi Kimara Suka, Omary Jumaa, anasema kwa sasa ng’ombe husafirishwa kutoka mikoani hadi Dar es Salaam, kwa kutumia magari ambayo kisheria hayakidhi matakawa ya kusafirisha mnyama.

Anasema wameshangaziwa na zuio la manispaa kusitisha shughuli za uchinjaji katika machinjio hayo, kwani limekiuka sheria za mnyama kwa kuwalazimisha wafanyabaishara kupeleka ng’ombe zao katika machinjio ya Pugu.

Wanasema hivi sasa, baada ya machinjio hayo kuzuiwa, ng’ombe hufikishwa hapo na kisha wanahamishiwa katika machinjio mengine kama ya Kimara Stop Over na Tegeta, ambako gharama ya uchinjaji iko juu, Sh. 50,000 kwa kila ng’ombe na athari zake ni nyama kuuzwa kwa bei ghali.

NAFASI YA WATAALAM
Matabibu wa mifugo wana wajibu wa kutoa tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya mifugo, kutoa elimu na ushauri kwa wafugaji kuhusu kanuni za ufugaji bora, pia kufanya ukaguzi wa nyama na ngozi na kutoaji wa vibali vya kusafirisha mifugo.

Takwimu zinaonyesha, mkoa wa Dar es Salaam kwa mwaka unazalisha wastani wa vipande vya ngozi za ng'ombe 194,489, mbuzi 72,788 na kondoo 18,948.

Pia kuna kilo za yama ya ng’ombe kilo za nyama ya ng’ombe 28,246,500 zinazozalishwa