Riadha watamba kuzinyoa Kenya, Uganda

26Apr 2016
Renatha Msungu
Dar es Salaam
Nipashe
Riadha watamba kuzinyoa Kenya, Uganda

KOCHA wa timu ya taifa ya riadha ya vijana (U17), Robert Kalihaye ametamba kuzigalagaza Kenya na Uganda katika mashindano ya Afrika Mashariki na Kati yaliyopangwa kufanyika Aprili 29-30 kwenye Uwanja Taifa, Dar es Salaam.

wanariadha: picha ya maktaba.

Akizungumza jana Kalihaye alisema alikuwa akizihofia nchi hizo kutokana na rekodi zao nzuri, lakini sasa hofu imepungua kutokana na wanariadha wake kuiva kimazoezi.

Alisema inaendelea kujifua ili kuhakikisha wanapata medali katika mashindano hayo.

Aliongeza kwa kusema amekuwa akiwapa wachezaji wake mazoezi asubuhi na jioni ili kuwaweka sawa na mashindano hayo.

Aliwataja wanariadha walio kambini Kibaha, Pwani kuwa ni Imani James, Benjamin Michael, Oscar Prosper, Adinan Haruna, John Silima, Sabas Daniel, Anton Mwanga, Elisha Wema, Jackson Makombe, Thobias Bura, Simon Francis, Emanuel Gadie, Francis Dambe, Hafidh Khalfan, Faraja Damas.

Kwa upande wa wanawake ni Rehema John, Jane Maige, Hynes Bampenja, Dorcas Boniface, Regina Deogratus, Bitrina Michael, Ester Martine, Eunice Musa, Rose Seif, Upendo Daniel, Mwanamina Hassan na Aisha Muhamed.