Azam FC yabakisha tatu kuvunja rekodi

26Apr 2016
Adam Fungamwango
Dar es Salaam
Nipashe
Azam FC yabakisha tatu kuvunja rekodi

TIMU ya Azam FC imebakisha mechi tatu za kushinda iweze kuvunja rekodi yake mwenyewe iliyoweka msimu wa 2013/14 ilipotwaa ubingwa kwa kushinda mechi 18.

Azam tayari imeshashinda michezo 16 mpaka sasa na inakamata nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Simba, ikijikusanyia pointi 55.

Timu hiyo imebakisha michezo sita kumaliza mechi 30 za Ligi Kuu Bara msimu huu inazopasa kucheza.

Wanalambalamba hao ni moja kati ya timu tatu ambazo zimo kwenye kinyang'anyiro cha kuusaka ubingwa Tanzania Bara msimu huu.

Mara ya mwisho timu hiyo kushinda mechi nyingi zaidi tangu ilipoanza kucheza ligi msimu wa 2013/14 iliposhinda mechi 18 na kutwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 62.

Idadi ya mechi chache zaidi kwa timu hiyo ilikuwa ni msimu wa 2008/09 ilipomaliza na kushika nafasi ya saba kwenye msimamo na kuzoa pointi 26.