Ninajali ubora wa kazi - Fid Q

10Mar 2016
Sabato Kasika
Dar
Nipashe
Ninajali ubora wa kazi - Fid Q

RAPA Farid Kubanda 'Fid Q' (pichani) amesema anapenda kufanya kolabo na wasanii wa nje wasio maarufu.

Fid Q

Alisema ameshuhudia wasanii wengi wa Bongo wakifanya kolabo na wasanii mashughuli kutoka kama Afrika Kusini, Nigeria, Kenya na Uganda kwa matumaini ya kutoka kimataifa.

"Lakini wanasahau kitu kimoja kwamba kinachotakiwa ni ubora wa kazi zao na siyo kufanya kolabo na wasanii mashuhuri," alisema Fid Q.

"Ndio maana kolabo zangu nyingi za nje nimefanya na wasanii wasio na majina akiwamo Taz kutoka Zambia." Aliwataka wasanii wa Tanzania kukizingatia kazi zao na kuepuka kutumia gharama kubwa.