Mkubwa na Wanawe wapigwa tafu

19Mar 2016
Frank Monyo
Dar
Nipashe
Mkubwa na Wanawe wapigwa tafu

KITUO cha kukuza na kuendeleza wasanii chipukizi cha Mkubwa na Wanawe ambacho kimeibua wanamuziki mbalimbali nyota wanaotamba, jana kilipokea msaada wa kompyuta tatu pamoja na kuunganishwa na huduma ya mtandao ya bure kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Yamoto bendi wakitumbuiza baada ya kupokea msaada.

Msaada huo uliotolewa na Kampuni ya simu ya Zantel na unatarajiwa kunufanisha wasanii 102 wanaojifunza muziki katika kituo hicho.

Akizungumza jana jijini, Ofisa Mtendaji wa Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema wameamua kutoa msaada huo baada ya kuona juhudi za kituo hicho kuwasaidia vijana wengi kutimiza ndoto zao kupitia sanaa.

Alisema msaada huo utawasaidia bendi ya Yamoto inayoongozwa na Dogo Aslay, Beka, Bella na Maromboso pamoja na vijana wanaojifunza sanaa katika kituo hicho.

Mwanzilishi wa kituo hicho Said Fella, alisema msaada huo utawawezesha vijana wanaofundishwa sanaa katika kituo hicho kujitangaza kitaifa na kimataifa kupitia teknolojia ya mtandao.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa kituo chake kinapokea msaada kutoka kwa wadau.