Amesema kuwa umefika wakati sasa wasanii wenzake kutumia muda wao mwingi katika kuboresha kazi zao ili waweze kufanya vizuri kwa vile ndiyo tiketi ya kuwafanya wafike mbali kikazi.
"Mimi sina nyimbo nyingi mpya, lakini hilo sio tatizo kwangu kwani katika shoo zangu za jukwaani huwa ninafuka na zinaonekana mpya kila siku, ndio maana ninawashauri wasanii wenzangu kubadilika," amesema Bushoke.
Msanii huyo amemshukuru Mungu na kusema kuwa siku zote anategemea kufanya kazi nzuri zaidi, ingawa alizonazo alizitoa siku nyingi lakini zinakubalika kila anapopata nafasi ya kutumbuiza.










