‘ANGEJUA’ yamrudisha kwa kishindo Dyna

24Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
‘ANGEJUA’ yamrudisha kwa kishindo Dyna

Msanii wa bongo fleva, Dyna Nyange ambaye ameibuka kwa kishindo na wimbo wake mpya wa ‘Angejua’ amesema kuwa kwasasa amelenga kutoka kwenye mipaka ya Tanzania na kufanya kazi nzuri ambazo zitamtambulisha upya kwenye soko la Afrika Mashariki.

Msanii wa bongo fleva, Dyna Nyange

‘Angejua’ ambayo imetengenezwa na kampuni ya kwetu studios chini ya msimamizi Msafiri Shabani imekuwa ikichezwa kwenye televisheni na radio mbalimbali huku baadhi ya wasanii wa njee wakiitangaza kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.

“ Ninafurahi jinsi kazi yangu ilivyopokelewa, Msanii kama Vivian wa nchini Kenya ameiweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kigeni lakini pia imekuwa ikisambaa kwa kasi kwenye vyombo vya habari,”alisema Dyna.

Kwa sasa Dyna amekuwa akijisimamia kwenye kazi zake baada ya kuachana na menejiment yake ya awali ‘Aljazeera’ lakini akasema, “Ukiwa chini ya menejimenti inayojielea utafurhai ila ukiwa chini ya menejimentii isiyojielewa basi utapata shida ni bora upambane na kupato kipato kizuri kwa kuteseka kuliko kupata kipato kidogo kisichoendana na hali halisi.