Young Killer kufunga ndoa karibuni

24Feb 2016
Na Mwandishi Wetu
Lete Raha
Young Killer kufunga ndoa karibuni

RAPA Young Killer, amesema kuwa siku yoyote kuanzia sasa anataka kufunga ndoa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Halimaty, vile hiyo ni moja ya ibada ya Mwenyezi Mungu na anaamini kwa kufanya hivyo vitu vingi vitamuendea sawa.

RAPA Young Killer,

Young Killer anayetamba na wimbo ‘Popote’ aliomshirikisha Juma Nature, amesema kuwa yeye na mpenzi wake wameshachunguzana na kudai kuwa sasa wanaweza kuishi kama mke na mume katika safari ambayo wanatarajia kuianza hivi karibuni.

Amesema kuwa hawezi kusema siku rasmi lakini muda siku yoyote ndoa inafungwa na kwamba mambo yake mengi yanabadilika kwenye maisha na kufafanua kuwa Mungu, anafungua milango kwa riziki.

Amesema anaamini kuwa hatua ya kufunga ndoa ina neema fulani na kwamba yeye na mpenzi wake huyo wanajuana vizuri na hawajakurupuka kuchukua hatua ya kuishi mum na mke.