Ni ishara nzuri ya namna ya kuwakwamua wananchi hao kiuchumi na kuwashirikisha katika harakati za kuinua hali ya uchumi wao.
Rais Magufuli amesema kuwa, uongozi wake hauna muda tena wa kupoteza katika kuhakikisha kuwa wakulima wa Tanzania wanainuliwa kutoka katika umaskini kwa kuhakikisha kuwa kilimo cha Tanzania kinaboreshwa haraka.
Amekuwa akirudia kila mara kusema kuwa wakulima wa nchi hii wameishi katika hali ya umaskini kwa miaka mingi kupita kiasi, na kwamba wameteseka sana.
Rais anasisitiza kuwa sasa ni mapambano ya ana kwa ana na umaskini wa wakulima maskini, kwamba hana muda tena wa kusubiri, serikali hii inakusudia kuongeza kasi ya kupambana na umaskini wa wananchi walio wengi.
Ni ukweli usiopingika kuwa dawa pekee ya kumwinua mkulima kutoka hapo alipo ni kwa kuinua thamani ya mazao ya kilimo.
Suala la umaskini linapozungumzwa linamgusa moja kwa moja mkulima, ingawa kwa bahati mbaya neema yoyote inapojitokeza ya bei nzuri ya bidhaa, hata kama juhudi zimetokana na mkulima mwenyewe, anayenufaika zaidi ni mfanyabiashara.
Bei ya bidhaa hupangwa kwa makubaliano kati ya mkulima na mlaji, lakini kwa kiwango kikubwa anayeathirika zaidi mwishoni mwa makubaliano hayo ni mkulima.
Ni wakati muafaka sasa serikali ikawa na mtandao utakaomgusa moja kwa moja mkulima ili naye anufaike na bei inayolingana na juhudi zake.
Kuwainua wakulima kutoka katika hali ya umaskini ni mikakati ambayo imekuwa ikibuniwa katika awamu zote za uongozi wa taifa hili, na nikutokana na kutambua umuhimu wa wakulima na kilimo kwamba ndio msingi wa maendeleo ya taifa.
Serikali kwa upande wake imejitahidi kusaidia gharama za mbolea pamoja na pembejeo nyingine, bado juhudi za makusudi zinatakiwa zifanyike kwa kuwafikia sehemu kubwa ya wakulima na kushauriana nao namna ya kuinua viwango vya uzalishaji wa mazao ya kilimo.
Dhamira ya serikali ya awamu ya tano ambayo sasa inalenga kukabiliana na umaskini wa maelfu ya Watanzania walioko vijijini ana kwa ana, ambao bado wanajikimu kwa mapato yatokanayo na kilimo duni, ni ishara nzuri ya namna ya kuwakwamua wananchi hao kiuchumi na kuwashirikisha katika harakati za kuinua hali ya uchumi wao.
Rais Magufuli amesema kuwa uongozi wake hauna muda tena wa kupoteza katika kuhakikisha kuwa wakulima wa Tanzania wanainuliwa kutoka katika umaskini kwa kuhakikisha kuwa kilimo cha Tanzania kinaboreshwa haraka.
Amekuwa akirudia kila mara kusema kuwa wakulima wa nchi hii wameishi katika hali ya umaskini kwa miaka mingi kupita kiasi, na kwamba wameteseka sana, anasisitiza kuwa sasa ni mapambano ya ana kwa ana na umaskini wa wakulima maskini, kwamba hana muda tena wa kusubiri.
Mwananchi anachotaka kujua kwanini bei za sembe, maharage, mafuta, sukari pamoja na nauli zinapanda bila kuzingatia hali ya uchumi wa mwananchi maskini huko vijijini!
Serikali inayo miradi mikubwa na pia vyanzo vingine vingi vya mapato ambavyo vinaweza kufidia kwa namna itakavyowezekana ongezeko la bei ya mahitaji ya msingi kwa wananchi wake.
Kodi zinazokusanywa zielekezwe pia katika kuziba ongezeko la bidhaa muhimu ili kumwondolea mwananchi wa kipato cha chini adha ya ugumu wa maisha haya.
Wafanyabiashara waachiwe uhuru wa bei huria kwa bidhaa nyingine kama nguo za mitumba nk. huduma muhimu ziwe na usimamizi madhubuti wa kuanzia serikali za vijiji hadi mijini, kusiwapo na mianya ya kuficha bidhaa muhimu kwa dhamira ya kutengeneza upungufu bandia ili hatimaye kuongeza bei ya bidhaa husika.
Inasemekana kuwa hata sukari ambayo hivi sasa katika maeneo mengi nchini inauzwa kwa bei ya shilingi elfu mbili, ni janja tu ya wafanyabiashara ya kusababisha uhaba usio halisi ili wapandishe bei.
Hali hiyo ingekuwa ngumu kama kungelikuwapo na mamlaka kisheria inayosimamia bei ya bidhaa muhimu kama hiyo sukari.
Wananchi wasiokuwa na kipato chochote sasa wanaishi katika hali ya utata sawasawa na mfanyakazi wa kima cha chini ambaye gharama za kumudu maisha yake hazilingani na fedha za mshahara wa kiima cha chini, anawajibika kwa gharama nyingi kama nauli yake na watoto wanaosoma, kodi ya nyumba, chakula, matibabu, nk.
Ni lazima mwisho wa mwezi ajikute na madeni makubwa ambayo hata haieleweki atayalipaje, ipo haja ya kupunguza manung'uniko na malalamiko ya wananchi kwa kubuni mikakati ya namna ya kupunguza makali ya maisha kwa wananchi wa kawaida na wale wenye kipato cha chini nchini.
Hatua mbalimbali za kubana matumizi ya fedha serikalini ni hatua moja tu ya jitihada za serikali za kuwasogezea wananchi huduma muhimu katika maisha yao.
Watanzania wengi wanapongeza jitihada za Rais Magufuli za kutoendekeza gharama za sherehe mbalimbali ambazo zinatumia fedha nyingi za walipa kodi bila tija, na hatua hiyo inaongeza dhana ya watendaji ya kuwajibika zaidi badala ya kusubiri mafungu ya fedha za matumizi kiholela katika maadhimisho, sherehe, makongamano, warsha nk.
Maoni: 0715-047304 na owdenkyambile@guardian.co.tz



.jpg?itok=nfwjwDzv)








