KACU yalipa malipo ya pili ya pamba Sh.milioni 186.3

17Feb 2024
Shaban Njia
Kahama
Nipashe
KACU yalipa malipo ya pili ya pamba Sh.milioni 186.3

CHAMA Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) mkoani Shinyanga, leo kimelipa malipo ya pili kwa wakulima wa zao la pamba waliokiuzia pamba msimu wa 2023/2024 kiasi cha Sh.milioni 186,316,776 hali itakayosaidia kuongeza uzalishaji.

Aidha malipo hayo yametolewa kwa wakulima wa Halmashauri za Msalala, Ushetu, Kishapu na Manispaa ya Kahama ambao walikiuzia pamba chama hicho na watalipwa Sh.36 kwa kila kilo moja, na wale wanauza pamba yao kwenye makampuni wanakosa nafasi hiyo. Kadhali, wakulima wa ushetu wamepata Sh.milioni 113,843,016 sawa na kilo milioni 3,162,306, Msalala kilo 241,760 sawa na Sh.milioni 8,703,360, Manispaa ya Kahama  kilo 159,960 sawa na Sh.milioni 5.758,560 huku wakulima wa kishapu wakiuza kilo milioni 1,611,440 sawa na Sh.milioni 58,011,840. Mwenyekiti wa KACU Tano Nsabi amesema wakulima hao walikiuzia chama jumla yap amba mbegu kilo milioni 5,175,466 na baada ya kuchakata na kuuza wanawalipa sehemu ya faida kiasi cha Sh.36 kwa kila kilo moja saw ana Sh,milioni 186,316,776 ambazo watazitumia kwenye maandalizi ya msimu ujao wa 2024.2025. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amesema kitendo kilichofanywa na uongozi wa kacu kinafaa kuingwa na vyama vingine vya ushirika ikiwemo SHIRECU na kinafanya kuwa na ushindani wa bei elekezi inayotolewa na serikali na kununua zaidi na wakulima kupata fedha. Amesema, kitendo cha ushirika huo kujitosa na kununua pamba kimesababisha kuwepo kwa ushindani wa bei na makampuni mengine na kuongeza uzalishaji pia mwakani msimu uliopita mkoa ulizalisha kilo milioni 10.4 za pamba na sasa umezalisha kilo milioni 38.