Kwa nini kuondoka kwa Messi PSG kutamgharimu Ballon d'Or

15May 2023
Na Waandishi Wetu
UFARANSA
Nipashe
Kwa nini kuondoka kwa Messi PSG kutamgharimu Ballon d'Or

KUJIONDOA kwa Lionel Messi katika Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) kunaweza kuharibu nafasi yake ya kushinda tuzo ya nane ya Ballon d'Or.

Mwandishi maarufu wa usajili, Fabrizio Romano, ameripoti kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

Wakati Messi amekuwa akihusishwa na kutaka kurejea Barcelona, kuna ripoti kwamba anaweza kucheza Mashariki ya Kati huku Klabu ya Al-Hilal ya Saudia ikimtaka na yeye ana nia ya kurejea Barcelona.

Wakati Messi mara nyingi amekuwa akikosolewa kwa uchezaji wake akiwa na PSG, Muargentina huyo alishinda Kombe la Dunia la FIFA la 2022 nchini Qatar. Hata hivyo, kuwaacha Paris kunaweza kuharibu uwezekano wa Messi kushinda Tuzo ya Ballon d'Or. Hapa, tunaangalia sababu tatu kwa nini hiyo inaweza kutokea...

 

#1 Kiwango cha uchezaji

Bado haijulikani ni wapi Messi atacheza msimu ujao. Iwe Barcelona, Mashariki ya Kati au klabu nyingine yoyote, haitakuwa rahisi kwa mchezaji huyo kuzoea klabu mpya.

Kipengele hiki kilionyeshwa wakati wa msimu wa kwanza wa Messi pale PSG. Alifanya vibaya, akifunga mabao 11 pekee na kutoa asisti 15 katika michezo 34 ya mashindano yote.

Kwa hiyo, hatua nyingine kwenye mazingira mapya inaweza kumfanya mchezaji apate shida. Hata hivyo, kutokana na kipaji chake, Messi anaweza kuthibitisha wakosoaji si sahihi.

 

#2 Kuhamia Saudia Arabia

Ingawa kuhamia Saudi Arabia kunaweza kuibua tena ushindani wa Messi na Cristiano Ronaldo, iwapo Ligi ya Saudia Pro League iko sawa na Ligi Kuu za Ulaya kunajadiliwa.

Hakuna shaka kuwa ligi inazidi kukua na uwapo wa Ronaldo umeipa umaarufu mpya. Ujio wa Messi unaweza kuongeza zaidi mvuto wa ligi. Lakini kwa upande wa mashindano, bado iko mbali na ligi tano Kuu za Ulaya.

Kwa hiyo, hata kama Messi kafunga mabao ya kustaajabisha kama Erling Haaland au Kylian Mbappe, bado hatakuwa kwenye ligi yenye ubora.

 

#3 Malumbano ya nje ya uwanja

Kama ilivyotajwa hapo awali, Messi alishinda Kombe la Dunia la FIFA la 2022 akiwa na Argentina. Alikuwa mshindi wa Mpira wa Dhahabu pia. Kwa PSG, amefunga mabao 20 na kutoa asisti 19 katika michezo 37 kwenye mashindano yote msimu huu.

Lakini hivi majuzi alipewa adhabu ya kufungiwa kwa wiki mbili na PSG kwa safari "isiyoidhinishwa" ya Saudi Arabia. Kuondoka kwake katika klabu hiyo ya Ufaransa kunaweza kuleta utata zaidi.

Hilo, pamoja na shutuma zinazowezekana kutoka kwa vyombo vya habari vya Ufaransa, vinaweza kuharibu nafasi yake ya kushinda Ballon d'Or, tuzo iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Ufaransa.