-tukio hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Triple-A mkoani Arusha.
Tukio hilo limehitimishwa jana, kufuatia kampeni ya miezi mitatu na kuwapata ma-DJ watatu kutoka kanda saba nchini.Mbali na zawadi hizo pia washindi wamepata nafasi ya kuwa ma-DJ rasmi wa chapa ya Serengeti Lite katika promosheni na shughuli zake za utangazaji wa bidhaa zao nchini.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Bia cha SBL, Nandy Mwiyombella, alisema, "Ni wakati wa kusisimua kwa SBL na bia yake ya kipekee, Serengeti Lite, ambayo imetumia shindano hili ili kuwasaidia vijana kuonyesha vipaji vyao. Serengeti Lite ina shauku ya kuwaona vijana kuonyesha umahiri wao katika vipaji walivyonavyo," alisema na kuongeza kuwa;
"Vilevile shabaha ya Take a Bite out of Life ililenga kutoa burudani kwa wateja wetu katika maeneo waliyopo ili waendelee kufurahia kinwyaji chenye ladha kamili cha Serengeti Lite, Bia ya Kitanzania iliyotengenezwa kwa ajili ya Watanzania na ya Watanzania," alisema
Afisa Vijana wa Arusha, Japhet Kurwa ndiye aliyeongoza hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa,John Mongella ambaye pia aliwatunuku washindi watatu waliobahatika. Kurwa alipongeza juhudi za SBL za kuchochea soko la ajira kwa kutoa motisha kwa vijana katika sekta ya burudani.

Kurwa alisema, "Nimejawa na furaha kubwa sana baada ya kushuhudia jinsi vijana wanavyopambania ndoto zao kwa nguvu na ari. Nawapongeza sana SBL kwa kutimiza ndoto zao. Ni siku nzuri kwa washindi hawa watatu; maisha yao hayatakuwa sawa tena kwa sababu fursa hii imekuwa chanzo cha ajira kwao. Nina uhakika pia kuwa washiriki wengine (hasa washindi) mtaanza kupokea mialiko mingi kwenye hafla za kutumbuiza mziki maeneo mbalimbali na pengine kufungua studio zenu za muziki hapo baadae.
Kurwa aliendelea kusema, "Tukio la leo limekuwa gumzo na kuibua hisia nzuri sana kwa vijana hapa mjini Arusha. Ni matumaini yetu kama Serikali ya mkoa kuwa vijana wamehamasika kujiinua kimaisha na kuchangamkia kila fursa zingine zilizopo ili kufikia malengo yao hasa katika hiki kipindi ambacho Serikali yetu inafanya kazi kubwa ya kuongeza ajira nchini’.
.jpg)
.jpg)
Kampeni ya Take a Bite Out of Life iliambatana na shughuli za burudani kutoka ma-DJs wa ndani walioshindana katika wilaya na mikoa nchini kote. Shindano hili lilishirikisha zaidi ya washindani 5,200 wenye zaidi ya miaka 18 wenye matarajio ya kujenga vipaji vyao kama waburudishaji wa muziki.
Katika kila tukio, washiriki waliobahatika waliondoka na zawadi mbalimbali na zaidi ya hayo jukwaa hili liliwapa fursa ya kuonyesha vipaji vyao mbele ya majaji maarufu kama vile DJ ZERO na umma kwa ujumla.
Hii si mara ya kwanza kwa SBL kuwekeza katika miradi kama hii. SBL pia imewekeza katika sekta ya michezo kwa kudhamini timu ya Taifa Stars, ligi ya Taifa ya Wanawake na mashindano mengine muhimu ya gofu.











