Msola alisema, “Paulsen ni kocha sahihi kwa timu ya vijana, alikuwa na mikakati mizuri, lakini TFF chini ya Rais wa zamani, Leodgar Tenga, ilichemka kumpa timu ya wakubwa ya taifa ‘Taifa Stars’ ambayo ilikuwa haiendani naye. Paulsen alikuwa na mipango mizuri ya kuendesha soka la vijana kwa kuratibu timu zote za klabu na akademia mbalimbali za vijana nchini.
“Ni kocha sahihi, ana uzoefu mzuri na anafahamu vipi ataweza kujenga soka letu kutokana na uzoefu wake. TFF inapaswa kumpa miaka isiyopungua minne ili aweze kufanya kasi yake kwa uhuru na kwa amani.
“Ninaamini litakuwa jambo sahihi kwani Paulsen analifahamu vizuri soka la Tanzania na anaweza kuleta mabadiliko kuanzia kwenye ngazi ya klabu hadi timu ya taifa,” alisema Msola.
Paulsen yuko nchini tangu wiki iliyopita na wakati wowote ule anaweza kusaini mkataba wa kuzifundisha timu za taifa za vijana yaani Serengeti Boys (U-17) na Ngorongoro Heroes (U-23).
Msola: Kocha Paulsen atatujengea soka letu
20Jan 2016
Lete Raha
Msola: Kocha Paulsen atatujengea soka letu
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Dk. Mshindo Msola, amelitaka Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kufanya maamuzi ya haraka ya kumpa mkataba kocha Mdernmark Kim Paulsen wa kuzifundisha timu za vijana za taifa ili aweze kulijenga soka la Tanzania .
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Dk. Mshindo Msola










