Coutinho ambaye pia ni nahodha wa klabu hiyo ya Malaysia alisema, “Ningependa kurejea Tanzania, hasa kwenye klabu za Simba au Yanga na hii inatokana na jinsi mashabiki wa timu hizo walivyo. Asikudanganye mtu, mpira bila mashabiki si kitu. Mimi binafsi nafurahia kucheza soka kwenye timu yenye mashabiki wengi.
“Natamani kurudi Yanga lakini sijui kama wananihitaji lakini pia ningependa kwenda Simba. Kama wananihitaji wanaweza kunitumia mkataba na kufuata utaratibu wa kuvunja huu nilionao huku na hilo halitakuwa na ubishi.
“Kilichokuwa kikinivutia Simba ni staili yao ya uchezaji yaani ni kama ya Kibrazili, pasi nyingi na soka la kuvutia. Nikipata nafasi kwenye klabu kama hiyo, hawataweza kujuta mimi kucheza huko. Bila shaka nitafanya makubwa,” alisema Coutinho.
Kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kufunga kwa 'fri-kiki', aliuzwa na Yanga mwishoni mwa mwaka jana kutokana na kutokuwa chaguo la kocha, Hans Van Der Pluijm.
Coutinho: Simba nipeni dili
20Jan 2016
Lete Raha
Coutinho: Simba nipeni dili
KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mbrazili Andrey Coutinho, ambaye kwasasa anakipiga kwenye klabu ya Myanmar iliyopo nchini Malaysia, amesema kuwa angependa kurejea nchini Tanzania kwaajili ya kuitumikia klabu ya Simba kama watamhitaji au kama Yanga wangependa kumrudisha kwa mara nyingine.
Mbrazili Andrey Coutinho.










