Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana jijini Dar es Salaam zinaeleza kuwa Atupele ambaye aliwahi kuichezea timu ya vijana ya Yanga na baadaye kujiunga na Kagera Sugar, amesaini mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza na gazeti hili jana, kiongozi mmoja wa Yanga alisema kuwa usajili huo umefanyika kwa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na Kocha Mkuu wa timu hiyo Mdachi Hans van der Pluijm.
"Kocha alisema anataka mshambuliaji mwenye nguvu na anayetumia akili, ukimuangalia Atupele ana sifa ambazo kocha ametaja katika ripoti yake," alisema kiongozi huyo.
Mabingwa hao wa Bara wamefanikiwa kumsajili Atupele kama mchezaji huru baada ya mshambuliaji huyo kumaliza mkataba wake wa mwaka mmoja wa kuitumikia Ndanda FC.
Kichuya ambaye pia ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kilichoko chini ya kocha Boniface 'Master' Mkwasa amesaini mkataba wa miaka miwili.
"Tayari tumeshakamilisha mazungumzo naye (Kichuya)," alisema kwa kifupi kiongozi huyo wa Simba ambaye pia ni Mjumbe katika Kamati ya usajili ya klabu hiyo.
Wekundu wa Msimbazi pia juzi usiku ilikamilisha usajili wa kiungo wa Coastal Union Hamad Juma kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Msemaji wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa klabu hiyo bado iko katika mazungumzo na nyota mbalimbali na watakapokamilisha, watatoa taarifa rasmi.
Wachezaji wengine ambao wanatajwa kuwaniwa na Simba ni kiungo Ibrahim Mohammed na beki Vicent Andrew 'Dante' wa Mtibwa Sugar, wote wamemaliza mikataba ya kuitumikia timu hiyo ya Manungu, Turiani mkoani Morogoro.










