Ujio wa Guardiola kumpa ulaji Mourinho Man U?

03Feb 2016
Nipashe
Ujio wa Guardiola kumpa ulaji Mourinho Man U?

UJIO wa Kocha Pep Guardiola Ligi Kuu England ni kama umebadili upepo kwa Manchester United, ambayo sasa inadhani jibu kamili la mabadiliko ya kocha kwenye klabu hiyo ni kumpa nafasi Kocha Jose Mourinho.

Kocha wa sasa Louis van Gaal yuko kwenye presha kubwa ya mahitaji ya ushindi na mabadiliko ya uchezaji wa kikosi hicho na mara kadhaa amekuwa akirpotiwa kutaka kutimuliwa. Manchester City wameingia mkataba wa miaka minne na kocha huyo wa Bayern Munich anayemaliza muda wake na mabingwa hao wa Bundasliga mwishoni mwa msimu huu. Man United sasa wa wakati mgumu wa kufanya uamuzi wa aidha, kubaki na mpango wake muda mrefu kumpa nafasi mkongwe Ryan Giggs au kumpa nafasi Mourinho. Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, Ed Woodward ambaye ndiye aliyeshika kisu cha fedha kwenye klabu hiyo, ana kazi ngumu ya kufanya uamuzi pengine kuliko wakati wowote. Tangu Kocha Alex Ferguson alipostaafu, Manchester City imeunda kikosi bora chenye nafasi ya kutwaa mataji kulinganisha na mahasimu wao City. Na ujio wa Guardiola utaiongezea uwezo City na kupanua umaarufu na mafanikio katika soka la kisasa na ushindani, lakini zaidi itawaacha mbali wapinzani wao Man United. Lakini kuja jambo moja linamsumbua Woodward, kwamba pamoja na CV nzuri ya 9l96k6kMourinho, lakini hakuna uhakika wa mafanikio kwa klabu hiyo mara kocha huyo Mreno atakapopewa nafasi hiyo.