IAAF yaongeza muda wa kufuzu Olimpiki

03Feb 2016
Nipashe
IAAF yaongeza muda wa kufuzu Olimpiki

SHIRIKISHO la Kimataifa la Riadha (IAAF) limeongeza muda wa wanariadha kuthibitisha kushiriki michezo ya Olimpiki, ambapo sasa mwisho ni Juni badala ya Machi mwaka huu kama ilivyotangazwa awali.

Hiyo imekuwa neema kwa wanariadha wa Tanzania na nchi nyinmgine, ambazo wanariadha wake walikuwa hawajafikia viwango vinavyotambulika na shirikisho hilo.
Akizungumza na gazeti hili jana Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) ili kutoa nafasi zaidi ya maandalizi kwa washiriki.
"Tunaishukuru IAAF kwa kuongeza muda wa kushiriki mashindano ya kufuzu, tutaitumia nafasi hii kuwahimiza wanariadha kufanya vizuri," alisema Zavalla.
Zavalla alisema wanariadha waliopo kwenye kikosi cha timu ya taifa ambao hawajafuzu kushiriki michezo hiyo, wajitokeze na kuitumia fursa hiyo.
Mbali na hilo, alisema kambi ya timu ya taifa ya riadha imehamishiwa mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza jana alisema wameamua kuhamishia kambi mkoani humo ili iwe rahisi kwa wanariadha kupata mahitaji yote muhimu ya maandalizi.