Wachezaji hao walikuwa Lubumbasi kwa wiki kadhaa kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa na taarifa rasmi ni kwamba wamefuzu. Meneja wa wachezaji hao, Jamal Kisongo alisema jana kuwa amepokea taarifa za kufuzu kwa majaribio kwa wachezaji hao kutoka benchi la ufundi la klabu hiyo. Kisongo alisema Ubwa na Chanongo wamefanya vizuri na kinachosubiriwa na mmiliki wa klabu hiyo kutoa uamuzi wa mikataba ya muda gani wanastahili kupewa. Kisongo alisema amefurahishwa na wachezaji hao kufuzu, kwani sasa kutaongeza ushindani kwa wachezaji wa Tanzania kusaka nafasi za kucheza soka la kuliowa nje ya nchi. "Nimeshapokea taarifa kuwa wachezaji wote wawili wamefuzu, kinachosubiriwa ni kusaini mkataba tu, kwa sasa Katumbi (Moise- Rais wa TP Mazembe) yupo nje ya Lubumbashi, anasubiriwa yeye kuamua," alisema Kisongo. Ubwa na Chanongo ambaye aliwahi kuichezea Simba, wanaungana na Ulimwengu na Samatta kuvaa jezi za Mazembe. Hata hivyo, baada ya kucheza kwa mafanikio Mazembe, Mbwana kwa sasa amechukuliwa na klabu ya Genk ya Ubelgiji na Ulimwengu bado anaendelea kuitumikia klabu hiyo.
Chanongo, Ubwa wafuzu TP Mazembe
03Feb 2016
Somoe Ng'itu
Nipashe
Chanongo, Ubwa wafuzu TP Mazembe
BAADA ya Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kukipiga TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), sasa ni zamu ya wachezaji Abuu Ubwa na Haroun Chanongo ambao wamefuzu majaribio na mabingwa hao wa Afrika.










