Twite aliyasema hayo baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya JKT RUVU ambao hawakuruhusu kufungwa.“Yanga ina wachezaji wengi wenye viwango sawa akikosekana mmoja mwingine anachukua nafasi yake hutuwezi kusema tumeshindwa kwa kuwa mchezaji fulani hakuwapo," alisema Twite.Tangu nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub, alipoumia Oktoba mwaka jana, kocha Hans van der Pluijm, amekuwa akimtumia Kelvin Yondani na Vincent Bossou kama mabeki wa kati kabla ya Yondani kufungiwa mechi tatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union.Timu ya Yanga bado inaendelea kushikirikia usukani wa ligi kuu Tanzania bara baada yakujikusanyia kibindoni pointi 43 hadi sasa.
Twite: Bila Yondani, Cannavaro tutapeta tu
10Feb 2016
Lete Raha
Twite: Bila Yondani, Cannavaro tutapeta tu
BEKI kiraka wa klabu ya Yanga, Mbuyu Twite, alisema licha ya kukosekana kwa mabeki wao wa kati nahodha Nadir Haroub na Kelvin Yondani, safu yao ya ulinzi haijatetereka.










