"Tuna kazi ngumu kwani Simba imekuja na kasi kubwa, tofauti na miaka mitatu iliyopita ambako vita ilikuwa ni dhidi ya Yanga tu, lakini sasa Simba imeibuka kwa kasi katikati ya ligi na presha imekuwa kubwa zaidi kileleni," alisema.Bocco alisema kudondosha pointi hivi sasa ni hatari na wanachopanga ni kucheza kila mechi kama fainali ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi. "Ligi ni ngumu, lakini tunapambana.Licha ya kuwa na mechi mbili za viporo, lakini hazitakuwa na faida hadi tutakaposhinda, kwani ukipoteza tu inakuwa imekula kwako. Hakuna ambaye anaweza kujihakikishia ubingwa kwa sasa," alisema.Alielezea kwamba njia pekee inayoweza kuwafikisha katika malengo yao ni umakini, nidhamu na kuzitumia vyema nafasi wanazopata.
Simba yapasua vichwa Azam
10Feb 2016
Lete Raha
Simba yapasua vichwa Azam
NAHODHA wa Azam, John Bocco, amesema klabu ya Simba, imeongeza presha kubwa katika harakati za kuwania ubingwa msimu huu tofauti na awali walipokuwa wanaitazama Yanga pekee.









