Msuva ampa mawazo Pluijm

10Feb 2016
Lete Raha
Msuva ampa mawazo Pluijm

KOCHA wa klabu ya Yanga, Mholanzi Hans van Pluijm, amemtaka winga wake, Simon Msuva, kuwa makini kwa nafasi za kufunga anazozipata ili kusaidia timu kupata magoli mengi.

SIMON MSUVA

Pluijm aliyasema hayo baada ya kushuhudia winga huyo akikosa nafasi zaidi ya sita huku akifunga magoli mawili katika ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya JKT RUVU, ushindi uliowaimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.“Msuva ni mchezaji mzuri ana kasi, ila tatizo lake kubwa ni umakini anapokuwa kwenye eneo la hatari la timu pinzani na ninakaa naye mara kwa mara ili kuliondoa hilo,” alisema Pluijm.Akizungumzia maandalizi ya mechi yao dhidi ya Cercle de Joachim ya Mauritius katika Ligi ya Mabingwa barani Afrika, Mholanzi huyo wanaipa umuhimu mkubwa mechi hiyo.“Tunafanya maadalizi sawa kwa kila mechi hatubagui hii ni ya kimataifa wala hii ni ya ligi tunahitaji kushinda kila mchezo ili tuweze kuwa mabingwa,” alisema Pluijm.Yanga inatarajiwa kuondoka muda leo kuelekea nchini Mauritius kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa wikiendi hii.