Wachezaji waliosimamishwa ni Riziki Juma wa Bandari Tanga kwa kosa la utovu wa nidhamu wakati Joseph Jackson wa JKT yeye ameshiriki ligi zaidi ya mbili katika jiji la Arusha na Dar es Salaam wakati Johaness John wa Oilers naye amecheza ligi mbili msimu huu.
John anatajwa katika ligi ya mkoa wa Dodoma na Dar es Salaam akiwa na timu tofauti.
Akizungumza na gazeti hili jana Mjumbe wa Kamishna ya Ufundi na Uendeshaji wa Mashindano, Manase Zabron alisema kamati hiyo imefanya uamuzi huo ili kutoa fundisho kwa timu nyingine kutorudia kosa hilo.
"Kwa mfano Riziki amesimamisha baada ya kutaka kumpiga mwamuzi, TBF imeshindwa kuvumilia utovu huo wa nidhamu na watasubiri adhabu nyingine," alisema Manase.
Alisema lengo la kuwaadhibu nyota hao ni kumaliza tatizo hilo na kuwaandaa kuwa wachezaji wa kulipwa kama ilivyotokea kwa baadhi ya wenzao waliopata timu nje ya nchi.










