Kocha Msaidizi wa kikosi cha wauza zabibu Dodoma jiji Fc, Kassimu Liyogope ametoa tambo hizo katika mkutano wao na waandishi uliofanyika ofisi za wadhamini wakuu wa ligi, Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mjini Geita.
Amesema kuwa wachezaji hao waliokuwa na majeraha tofauti wameshaanza mazoezi na kuonyesha utimamu wa kimwili na kiakili na hiyo inaashiria kuwa wataongeza nguvu ya timu kusaka alama hizo tatu muhimu.
“wachezaji wetu ambao walikuwa majeruhi, na wale ambao tuliwamiss tangu ligi imeanza kesho wote watakuwepo, kwa hiyo tutarajie kutakuwa na sura mpya na nguvu mpya uwanjani hivyo tunategemea kupata matokeo mazuri .
Aidha amesisitiza kuwa wamejipanga kutumia mchezo wao wa jumamosi dhidi ya Geita Gold ya mjini Geita kusafisha makosa yaliyopelekea wao kutofanya vizuri katika michezo yao iliyopita ili kurejesha molari ya timu yao .
Nahodha wa Dodoma Jiji Fc, Augustino Nsata alikiri mchezo wao dhidi ya Geita Gold ni mgumu lakini msimamo wa ligi unawapa hamasa ya kupamabana kupata matokeo mazuri ili wasoge juu zaidi.
Kocha Msaidizi wa Geita Gold, Ally Magazija alisema wamejipanga kurejesha heshima ya uwanja wa Nyankumbu kwa kuhakikisha wanachukua alama zote tatu za mchezo wa kesho dhdi ya Dodoma jiji.
Kiungo wa timu ya Geita Gold, FC Samweli Nditi amesema kuwa matokeo ya mabaya ya michezo mitatu iliyopita yamewaamsha na kuwaongezea ari ya kupamabana zaidi ili wapate matokeo mazuri ya michezo inayofuata ukiwemo wa kesho .










