Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo Mkurugenzi wa duka la Mr Discount Khalid Mbarak alisema wameamua kumtangaza bondia huyo kutokana na kuridhishwa na utendaji wake wa kazi pamoja na nidhamu aliyokuwa nayo.
"Nidhamu ndio kila kitu tumeamua kumpa ubalozi mandonga kutokana na kuridhishwa na nidhamu pamoja na utendaji wake wa kazi,alisema.
Alisema mbali na Mandonga vile vile watawapa ubalozi wachezaji wengine wakiwemo wa riadha,mpira wa miguu,Wakati huo huo karim Mandonga aliwataka mabondia pamoja wachezaji wote nchini kuwa na nidhamu kwani nidhamu imemfanya afike mbali kwenye mchezo wa ngumi na kuahidi kufanya kazi yake hiyo kwa nguvu moja.
Alisema amefurahi kupata ubalozi huo na kusema atapambana kuhakikisha anafika mbali kupitia ubalozi huo.









